WANAWAKE WANATAJWA KUWA WAATHIRIKA WAKUBWA WA MABADIRIKO YA TABIA NCHI



PICHA: Wakulima Wanawake Wakiwa Wanalima Kilimo Cha Mkono na Jembe

WANAWAKE WANATAJWA KUWA WAATHIRIKA WAKUBWA WA MABADIRIKO YA TABIA NCHI

Na Emmanuel Chibasa.

Tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa Wanawake wanatajwa kuwa katika hatari na athari zaidi zinazotokana na mabadiriko ya tabia nchi kutokana na Mazingira ya umasikini pamoja na uwezo wao wa kukabiliana na majanga pamoja ushiriki wao katika nafasi za Kufanya maamuzi.

Katika kipindi hiki ambacho Dunia inaendelea kushuhudia athari za mabadiriko ya tabia nchi, Wanawake nao wanatajwa kuwa na nafasi muhimu katika kusaidia Kudhibiti athari hizo lakini kuna mambo ambayo yanahitajika Kufanya Ili Kutoa fursa kwa Wanawake kushiriki katika mabadiriko ya tabia nchi.

Rebeka Muna kutoka jukwaa la Mabadiriko ya Tabia nchi Tanzania la forum cc anasema Wanawake wanatajwa kuwa waathirika wa madiriko ya tabia nchi kutokana na nafasi walionayo katika Jamii 

Kuwa ni kundi dhaifu na kutoshirikishwa katika maamuzi, taarifa dhaifu na athari za Mila na Imani hivyo kuathiri njia za kujipatia kipato

Wanaharakati wa haki za Wanawake wanasema Kuna umuhimu mkubwa wa Kuvunja vizuizi vikubwa vya kiimani, utamaduni na kuhusisha kwenye maamuzi kukabiliana na Mabadiriko ya Tabia nchi sababu Athari hizo zinawagusa Moja Moja katika Kilimo, Hali ya kiafya, Kijinsia na kijamii.

Ushiriki Wanawake katika kukabiliana na athari za mabadiriko ya tabia nchi bado ni mdogo lakini wakishirikishwa katika mipango na sera wanaweza kuleta suluhisho katika kukabiliana na Athari hizo kwanza Kwa wao kujiamini, Jamii kuachana na utamaduni na imani zilizopitwa na wakati, kupata taarifa, kuwapa nyenzo, teknolojia pamoja na kupewa nafasi za maamuzi katika ngazi mbalimbali

First Story
Like this story?
Join World Pulse now to read more inspiring stories and connect with women speaking out across the globe!
Leave a supportive comment to encourage this author
Tell your own story
Explore more stories on topics you care about